Baadhi ya wasanii kutoka Dodoma wameshiriki katika wimbo wa pamoja unaokwenda kwa jina la "TWAWAKUMBUKA" au "Rest In Peace" kuwambuka baadhi ya watu waliopoteza maisha, hasa vijana katika project iliyoitwa DTP ama Dodoma Tupo Pamoja iliyoongozwa na mmiliki wa website ya Capital Tz ndugu James Msofe, ambae kwa sasa yupo nchini Sri Lanka kimasomo.
Wimbo huo hasa umewalenga Matei Mmassy (aliyekuwa mmiliki wa Matei Lounge & Car Wash, Area D, Dodoma), Joshua Oguda (wakili/mwanasheria na mkufunzi wa chuo cha St John) na Chid Nyau waliofariki kwa ajali ya gari mwezi 11, 2014, waliokuwa wakitokea Morogoro kwenda Dodoma.
Wasanii walioshiriki katika wimbo huo ni pamoja na Raph Tz (aliyeongoza ufanyikaji wa wimbo huo), Big Born 90, Bizo Mc, One Six, Mekstar, Uncreakable, mwanadada Chubby, L5, Jimmy Yeyoo, Brezy, Bushman na Jaco Beatz.
Pia utangulizi (INTRO) umefanywa na muongozaji wa video Erick Backamaza na hitimisho (AUTRO) umefanywa na Willz Snady (mtangazaji wa redio Impact Fm 94.4 Dodoma)
Wimbo umefanywa na Kid Man wa B1 Records, Makole Dodoma.
0 comments:
Post a Comment