Thursday, 4 December 2014

Instagram media by bossngasa - Daaa... R.I.P @mateymmassy @onjikooguda ...Ni ngumu kuamini na mpk muda huu bado cjaamini..Daaa....
Wekeend iliyopita Gari aina ya Mack x tulipata nayo ajali,Ambapo tulikuwa watu wa tano ndani ya gari hiyo,tulikuwa tunatokea  Morogoro kwenye msiba wa rafiki yetu mpendwa ambaye ni maaufu kwa jina la chidy Nyau.Ajali hiyo ilitokea majira sa 12 mbili ambapo chanzo cha ajali hiyo mimi nikiwa kama mhusika niliyekuwemo ndani ya gari hiyo kiukweli sikumbuki hata kidogo... kitu ambacho nimeweza kukumbuka ni kwamba nilikuwa usingizini na nimekuja kushtuka ajali imeshakwisha kutokea... baada ya hapo nilizinduka gafla kutoka usingizini na kufungua mkanda niliokuwa nimefunga na mlango nikafungua mwenyewe na kutoka... Ndugu yangu mpendwa Matei John Mmasi ambaye ni mfanya biashara maarufu mjini Dodoma  alipoteza maisha pale pale  huku Joshua uguda ambaye ni lecture wa chuo cha st john Dodoma aliumia vibaya kichwana na sehemu za kifua na masaa machache alipoteza maisha akiwa hospitali ya Rufaa Dodoma (Generali) Huku kijana mwingine ambaye alikuwa amekaa siti ya nyuma kati kati aliumia sana sehemu ya mikono yake ..Yani Nyama zote zilitoka kwenye mkono wa kushoto na kulia.. Mwingine aliyekuwepo kwenye ajali hiyo Anafahamika kwa jina la Hassani Gobosi ambapo na yeye anaendelea vizuri pamoja na Boss Ngasa:EEE mungu ilaze roho za marehemu mahali pema peponi

Source: BOSS NGASA TZ

1 comments:

  1. Sijaona chanzo kama kichwa cha habari kinavyovuta uingie kusoma. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu na poleni kwa mlioumia katika ajali hiyo.

    ReplyDelete