Salim Kikeke ni mtangazaji kinara wa BBC Dira ya Dunia TV. Safari yake ya utangazaji ni ndefu, ilichipuka miaka ya 90 akianzia redio na baadaye televisheni ambapo alipitia CTN, DTV na ITV.
Salim ambaye ni mtanzania, alielekea Uingereza mwaka 2003 akitokea kituo cha televisheni cha ITV jiji Dar Es Salaam, akiwa London alitangaza na kusimamia matangazo ya Dira ya Dunia, Amka na BBC na hata BBC Ulimwengu wa Soka.
Amejipatia umaarufu mkubwa kote inakotazamwa BBC Dira ya Dunia TV na hata kushinda tuzo kwa uhodari wake.Lakini mambo yalizidi kunoga mwaka 2012 wakati aliteuliwa kuwa mtangazaji kinara wa BBC Dira ya Dunia TV. Ilikuwaje akapata fursa hiyo, gonga video hapo chini upate maelezo kamili.
0 comments:
Post a Comment